Tuesday, May 29, 2012
Mwenge wa uhuru waendelea kukimbizwa.. upo Mbinga
Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Nyasa Bi Happy Msanga (kushoto)
akikabidhi Mwenge wa uhuru kwa Kaimu Katibu Tawala wilaya ya Mbinga
Bw.Iddi Mponda baada ya kumaliza mbio zake katika wilaya ya Nyasa.Tukio
hili limefanyika leo katika kijiji cha Chunya wilaya ya Mbinga
BASATA YAWATAKA WASANII KUONGEZA THAMANI KATIKA KAZI ZAO
Huku kukiwa na juhudi za kutambuliwa
na kuthaminiwa kazi za wasanii ndani na nje ya nchi, Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA)
limewataka wasanii kuongeza thamani kwenye kazi zao ili
kuzipa ubora zaidi.
Wito huo umetolewa mapema
wiki hii na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari wa BASATA Godfrey
Lebejo wakati akihitimisha programu maalum iliyohusu Ubunifu, Utengenezaji na
Uongezaji thamani katika
Kazi za Sanaa kupitia Jukwaa la Sanaa.
Alisema kuwa, ubora
katika Sanaa unapatikana pia kwa Wasanii kuangalia wenzao wanafanya nini na wao
kupata ubunifu mpya kwa kuongeza vionjo, uthamani na ubunifu binafsi katika
kuifanya
kazi ya Sanaa kwanza
kupendwa na baadaye kupewa thamani kubwa sokoni.
“Ni wazi Wasanii wetu wanapaswa
kuzingatia uongezaji uthamani kwenye kazi wanazozifanya. Kubuni kazi ni suala
moja lakini kuongeza uthamani katika kazi yako ili ivutie wengi na
kuuzika kwa thamani kubwa
ni suala lingine la kuzingatia” alisistiza Lebejo.
Aliongeza kuwa, kwa sasa kuna
taarifa za Wakenya kununua kazi za Wasanii wetu kwa bei ya chini na
baadaye kuziongezea
ubunifu, thamani na kuziuza nje kwa bei kubwa. Katika hili
anasema, inatokana na wasanii
wetu kutokuzingatia falsafa hiyo ya ubunifu na uongezaji thamani wa
kazi zao.
kutumia ipasavyo
malighafi hizo katika kubuni kazi zenye ubora na kuhakikisha
tunazipa thamani stahiki
tunapozisafirisha nje” alizidi kusisitiza.
Awali akiendesha darasa hilo
maalum ambalo wiki hii lilikuwa mahsusi kwa ajili ya wasanii na
wajasiriamali wa Sanaa za
mikono (Handcrafts), Haroun Sabili kutoka asasi ya
Musoma Handcraft alisema
kuwa, Sanaa hizo zinahitaji ubunifu na umakini mkubwa
kwani kinyume chake ni
kutokuvutia na kupoteza uthamani.
Alitoa wito kwa Wasanii kujiunga
katika vikundi na kuwa rasmi ili kuhakikisha kwanza,wanajenga
mazingira ya kuwezeshwa lakini
pia kupata mafunzo mbalimbali ambayo yatawafanya
wazalishe kazi za Sanaa
zenye ubora na thamani kubwa.
“Ni ngumu sana kuhudumia msanii
mmoja-mmoja lakini mkiwa kwenye umoja ni rahisi sana kupata fursa za uwezeshaji
hususan mafunzo katika kuongeza ubunifu na uthamani wa kazi zenu”
alishauri Haroun.
Katika programu hiyo iliyohudhuriwa
na wadau 72, elimu kuhusu ubunifu na uongezaji thamani kwenye
kazi za Sanaa ilitolewa
sambamba na malighafi mbalimbali na jinsi zinavyoweza
kutumika kuzalisha kazi
za mikono kuoneshwa.
MEDIA BRIEFING NOTE FOR THE GLOBAL 2013 SMART PARTNERSHIP DIALOGUE TO BE HELD IN DAR ES SALAAM, TANZANIA – 24TH TO 28TH MAY, 2013
Tanzania will host the
next Smart Partnership Dialogue that is scheduled to take place from 24th to
28th May, 2013 in Dar es Salaam. President Jakaya Mrisho Kikwete, is
expected to officiate the National launch at noon today
Tuesday May 29, 2012 at the Karimjee Hall grounds in Dar es salaam.
President Kikwete had
agreed to host the event during the last dialogue that took place in
Putrajaya, Malaysia in June, 2011 - branded the Langkawi
International Dialogue.
The Smart Partnership
Dialogues are a brainchild of the Commonwealth Partnership for Technology
Management. The CPTM which is the social and scientific interlinkage arm of the
Commonwealth, has since 1995 undertaken in collaboration with willing national
partners to provide a forum that cuts across the east-west, have, have not’s
and the developed and developing dichotomy for the discussion of topical
subjects in a conducive inclusive, open dialogue. Inspired by the increasing
need to ensure a win-win interrelationship between actors, the CPTM, in
collaboration with the host country undertake to provide an ambient setting where
individuals from all walks of life and professions can meet and hold serious
discourse on selected subjects every two years.
To
ensure that these dialogues are successful, a two pronged approach is utilized.
The first is when the host country convenes a National
Dialogue. This involves the gathering together of different sectors of the host
community and coming up with a topical issue that is not just locally relevant,
but which resonates internationally and merits a grander discourse and focus.
The second is when the Host country in collaboration with
the CPTM plan for, invite participants and hold an international open dialogue
on the selected topic, in essence, host aSMART DIALOGUE.
As hosts, the kicking
off of the National Dialogue is very crucial. It is a means for creating
National and International awareness of the next host of the Dialogue and
avails the opportunity to announce the dialogue venue, topic and dates.
The
Launch of the National Campaign for the Dialogue in Tanzania will take place on
the 29th May, 2012 at the Karimjee Hall Grounds from 10:00 am to 11:00
am. The Host and Patron Advisor for the 2013 |Smart Partnership
Dialogue, H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of
Tanzania will officially launch preparations for the 2013 Dialogue and
introduce the Theme for the Dialogue (Leveraging Technology for
Africa’s Socio-Economic Transformation) announce the date for the
Dialogue (24th to 28th May, 2013) and the venue (Dar es Salaam) issue a holistic invitation to both
the citizens of Tanzania as well as the International Community at large, and
share his vision for the Dialogue. The Dialogue has been branded the GLOBAL 2013 SMART PARTNERSHIP DIALOGUE in anticipation
of interest the chosen theme is likely to raise. Technology is a global
phenomenon, a global concern, a global topical issue. It is therefore more than
likely that a Dialogue on Technology for development shall merit global
attention and have a global audience/participation.
The Execution of the
preparation will be undertaken under the guidance of the Chief Secretary who is
the Convener of the Dialogue. The Chief Secretary will be supported by a
National Steering Committee that comprises of Permanent Secretaries from All
Ministries as well as Representatives of Keyline Sectors both on Mainland
Tanzania and Zanzibar.
A Focal Point Team from
the Ministry of Foreign Affairs will spearhead the logistical and liaising
activities necessary for the successful execution of the Dialogue. The Team
will over time incorporate Members from different Links
A Resource Group with
an Advisory role comprising of key members of the Academia, Business and
Corporate Community, Youth, Labour, Culture, Industry and Media has been set up
under the leadership of Professor Samuel Wangwe.
Following the National
Launch, the next step is scheduled to be contact with different Links within
Tanzania who will in turn be linked with counterparts interested in
participating in the Dialogue in 2013. A National Dialogue to discuss the theme
will follow thereafter.
Other African countries
that have hosted the Smart Partnership Dialogues include Botswana, Namibia,
Zambia, Zimbabwe, Mozambique, Swaziland, Lesotho and Uganda that has hosted it
twice. Other countries include Barbados, and Malaysis that has hosted the
dialogue nine times.
Issued by
THE FOCAL POINT TEAM, GLOBAL 2013 SMART PARTNERSHIP
DIALOGUE, MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION
Monday, May 28, 2012
RAULA Filamu itakayokimbiza
KUNA filamu inakuja ,
ambayo kwa kuangalia tu mshikemshike wake kwenye uchukauji lazima ije kuwakimbiza
watu.
Utata mtupu,
mazingira matata matupu, uchokara lakini
dhuluma na makasheshe behind the
Scene itakuwa noma. Watu wanazimia Scene kali kwelikweli.
| Chuchu akiwa katika jeneza |
| hapa ndipo scene ilipoanza kuwasha |
| Hii ikawa taabu kwelikweli. Huyo ni Raula, mtoto halisi wa Chuchu |
Naam hiyo itakuwa
tamu manake hata Nyota wa filamu wa kike
nchini Chuchu Hansi alijikuta akiangua kilio kizito baada ya kumaliza scene ya kuingizwa
kwenye jeneza ambako mtoto wake naye anaigiza na alitoa unyende babu kubwa.
Chuchu aliagiza kama mnke wa mtu aliyekufa aliyeteswa na kufa
kwa mateso.
Kasheshe ikaja pale
alipolala kwenye jeneza, baada na watu kuja kuga mwili wake, ndipo
mwanaye kipenzi Faria (anayeigiza kama Raula) alipolia kinoma.
Raula alilia kwa
hisia kali huku akiita mama!! Mama!!, na kung’ang’amia jeneza huku akitiririkwa
na machozi. Hisia kali zilipenya maskioni mwa mama yake wakati wa Scene na
kumfanya kushindwa kutoka kwa kilio na kuishiwa nguvu baada ya kumaliza
shooting.
Hii sinema we acha
tu,Mwigizaji mwingine wakati akiaga (duhh inayotakiwa kuwa maiti ya Chuchu),
akiigiza kulia ghafla aliregea na kudondoka chini, hali iliyopelekea watu
kwenda kumuokota na kumweka vizuri.
Tofauti ilivyokuwa
kwa Chuchu, kwani mwanamama huyo alipooza kabisa fahamu na kupata tabu katika
upumuaji.
Ilimbidi kumchukua na kuandaa chumba maalum kwaajili ya kuweka
waliozidiwa, ili kumrudisha katika hali yake ya kawaida. Ilimchukuwa
zaidi ya dakika 45 katika kuzinduka na kuwa katika hali ya kawaida huku maombi
makali yakipigwa katika kuhakikisha anarudi kuwa sawa.
Mauzauza
hayakuishia hapo, hadi kwa mwigizaji maarufu na mkongwe Rachel ambaye
alishaigiza filamu nyingi za kulia, lakini hapo alijikuta akizidiwa kiasi cha
kulia mpaka kupata maumivu makali ya kichwa. Naye ilibidi achukuliwa
haraka na kupelekwa kwenye chumba maalum kwaajili ya kupata huduma, kwani
alikuwa akilalama kwamba hali yake sio nzuri kabisa, kutokana na maumivu ya
kichwa.
Kwa habari
zaidi nenda http://www.bongounit.blogspot.com
ZANZIBAR HALI SI SHWARI
![]() |
| MADHEBAHU YA KANISA LA T.A.G KARIAKOO ZANZIBAR |
![]() |
| UPANDE WA MADIRISHA YA KANISA LA T.A.G KARIAKOO ZANZIBAR |
![]() |
| UPANDE WA MADIRISHA YA KANISA LA T.A.G KARIAKOO ZANZIBAR |
![]() |
| MABAKI YA VITU VILIVYOTUMIKA KURIPULIA KANISA HILO |
![]() |
| MCHUNGAJI DICKSON KAGANGA WA KANISA LA T.A.G KARIAKOO AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KANISANI HAPO |
![]() |
| WAUMINI WAKIWEKA SAWA MABAKI |
![]() |
| MCHUNGAJI DICKSON KAGANGA WA KANISA LA T.A.G KARIAKOO AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KANISANI HAPO |
![]() |
| UFA ULIOSABABISHWA NA MRIPUKO |
![]() |
| WAUMINI WAKIJADILI JAMBO NYUMA YAO KUKIWA NA BAADHI YA MABAKI VIKIWEMO VITI |
![]() |
| WAUMINI WAKIZIBA MADIRISHA TAYARI KWA IBADA |
![]() |
| GARI ILIYORIPULIWA NDANI YA ENEO LA KANISA LA T.A.G KARIAKOO ZANZIBAR |
![]() |
| KANISA LA T.A.G KARIAKOO LIKIWA KATIKA HALI MBAYA |
![]() |
| ASKARI WA KUTULIZA GHASIA AKIWA KAZINI MJINI ZANZIBAR |
![]() |
| MAENEO YA MICHENZANI MATAIRI YALICHOMWA |
![]() |
| ASKARI WA KUTULIZA GHASIA LEO ASUBUHI WAKIHAKIKISHA USALAMA UNAKUEPO |
![]() |
| HUO NI MOSHI WA MATAIRI UKIWA UMECHANGANYIKA NA MABOMU YA MACHOZI |
![]() |
| HAPO NI HARAKATI ZA KUTULIZA GHASIA |
![]() |
| MICHENZANI USIKU WA KUAMKIA LEO |
![]() |
| MICHENZANI PAKIFUKA MOSHI |
![]() |
| MSHIKE MSHIKE |
Beda Msimbe reflections :mwenye akili na asiyekuwa na akili kwa kawaida lao moja
KWA sasa Tanzania imeingia katika wimbi kubwa la kushabikia
matatizo yanayoambatana na ufujaji wa fedha, wizi, rushwa na ufisadi; zipo pia
kauli mbalimbali zinatolewa kuhusiana na matatizo hayo, chimbuko lake na laana
inayoambatana nayo.
Mimi sina shaka na kampeni hii ya kuondoa udhalimu katika
maisha ya watu ila nina mashaka na wimbo huu unavyoimbwa, wapo watu wanataka
zari na wala si shari na hili lazima
niliseme.
Yapo madai kuwa waandishi wa habari ni kioo cha jamii. Lakini
bila kujali uprofesheni au la, waandishi ambao kihistoria wapo tangu enzi za
kale katika majina tofauti ni watu hatari sana wanapoamua kufanya mambo kiutata
hasa pale wanapoamua kwa makusudi mazim akushabikia au kutoa habari iliyopwelea
vitu kibao.
Bila hata kuuma meno
kwani na mie nimo (inafaa wakati mwingine kumla jongooo kwa kung’ata
meno mbichi) tunachekelea hatari kwa kuandika vilivyonusu nusu na kupeleka kwa
jamii ambayo inatarajia tuchambue na
tuwape nafasi wao waamue na si kwa kuwapeleka kama maiti kwenda kuzikwa.
Kwa ufupi tunaifanya jamii kuwa yenyewe haina daraja, haijui
vibaya na ambayo haiwezi kuchambua mambo wala kujenga msingi mzuri wa kuelewa
chimbuko na kutafuta mgogoro wake.
Kama utaangalia sentensi ya kwamba, ukichambua magazeti hata
yale uliyosoma wiki hii utatambua kwamba kioo hiki cha jamii kina walakini,
kina tope na wote tunaojitazama tunajiona kuwa tuna tope kumbe tupo waa bila
doa.
Naam, watu wanadhani ni masikhara lakini kalamu ni silaha
mbaya kuliko hata bomu la nyukilia. Bomu likiua kifizikia,kalamu huua kiakili
na kumfa nya mtu asiwe kabisa na haja wala nia ya kufanya vitu vyenye maana
duniani akibaki kuwa mbeya na shambenga mkubwa.
Mimi ningelipenda kuzungumza sana kuhusu ushambenga na umbeya
kwani si ndivyo ilivyo?!
Mathalani miaka ya karibuni Wasauzi walikuwa na jihadi ya aina
yake waliwashambulia wageni kwani wamewapoka utajiri wao. Kimsingi mashambulio
hayo unaweza kuyaona kama yanatokana na matatizo ya kiuchumi lakini kiutaalamu
ni tatizo la kisosho kwani kimsingi
wakishamalizana na wageni ambao ni
waswahili wenzao watawaibukia, wazungu na wahindi na wakishawamaliza wataanza
kuwaangalia Wakosa na Wazulu kisha nani ni nani katika makabila ya
wenyewe.Itakuja wewe si wa ukoo wangu.Nataka kusema ile ni dhambi ya ubaguzi
Habari ndio hiyo.
Nasema ndio hiyo kwa kuwa matatizo mengi ambayo yamesababishwa
na magazeti ambayo yametengeneza kuwa wageni (huko) wanashika nafasi ya kazi na
wenyeji wanakosa huku wakisahau kuwa kila Ijumaa wanapokea fedha za kazi na
hawarudi kazini mpaka fedha hizo zimeisha Jumanne.
Pia wanasahau kuwa wao wakishapata fedha hawarejei nyumbani
kabisa na wala watu wao hawawezi kuwa na akiba ya fedha za maendeleo, watoto
hawaendi shule na watanzania waliodhamiria kubadili maisha wanakubali kulala
katika maguni na kurejesha fedha nyumbani.
Mimi naamini nikikumbuka, magazeti na vyombo vya habari local
vimechangia sana mtafaruku ule, ndio maana nathubutu kuuliza kioo kikiingia
uchafu inakuwaje vile?
Wanawake wa Afrika kusini wapo tayari kubembelezana na
wahamiaji kwa kuwa wanajua wanafanya nini, wanataka nini na wanawajali lakini
si wanaume wao ambao umkomboti ndio dawa inayotitibua ufanisi katika kazi.Haya
si matusi ni mifano halisi tu katika jumuiya.
Naam hao ni waafrika kusini tatizo la kijamii wameligeuza la
kiuchumi na kuwaswaga wenzao, dhambi hizo ama hakika zitawarejea hata wao kama
mwalimu Nyerere alivyokwishawahi kusema mkishamaliza huko pembeni hakika
mtarejea nyumbani mkamalizane.
Dhambi ya kula nyama ya mtu si ya kawaida, kwani lazima
itaendelea kutafuna wengine.
Tuache hayo ya mathalani ya Afrika Kusini turejee hapa
nyumbani Hivi.Wakati mwingine ni kweli kuwa tunaandika tukitambua kwa kufanya
hivi tunahatarisha vitu vingi, lakini tunasukumwa tukiamini kuwa ustawi wa
taifa ndio dira kumbe unakula kasumba ambayo ungeliifua zaidi ungelitambua
kwamba ni bangi la kukupumbaza.
Wapo watu wanatoa hoja uchwara kuhusu ufisadi, kuhusu rushwa
na kuhusu mambo mengi ambayo kimsingi hayana maana kusimuliwa lakini tugeuza
gumzo tunaacha kitu cha msingi.Ndio inawezekana kabisa, lakini je umeshajiuliza
maswali kadhaa kabla hujatoa konklusheni?
Swali la kwanza nini laifu staili ya mtu?
Swali la pili nini kinamfadhaisha mtu katika maisha yake?
Swali la tatu unajua kwamba si kila mgonjwa hufa mara moja
lakini kila mzima hufa dakika ile ile anayotakiwa kufa?.
Nani alisema kwamba
ukiugua huruhusiwi kufa na pia ukiwa mtu mzima huruhusiwi kufa?
Je kama ni kweli kuwa kufa lazima kuwe na sababu na anayeliwa
na simba ni nani kachonga mingo ya mauaji?
Ningelipenda usinielewe kabisa, kwani ukinielewa hutaleta
shida.Waandishi wa habari tunaweza kuleta
shida sana katika maisha kama kila kitu tutakichukua kama kilivyo halafu
mseme kwamba kuna mkono wa mtu. Nina shaka kubwa huu mkono wa mtu si wa kweli.
Huenda hali ya mashaka inatokana na waandishi wa habari
kuchukua sana maneno ya mitaani, kutochambua inavyostahili na kushikilia
maelekezo mzunguko yanayofanywa na maspinidokta ili mradi waue sooo wanayotaka
kwa kupakazia upande mwingine, wataalamu wa lugha za kifisadi wanasema ni
blackmail.
Halafu si unajua tena kuna matangazo mengi, haya magazeti ya
kwenye mitandao ambayo inawafanya watu kitu mbaya kabisa.Inachukua tu yenyewe
si watu wanaposti, lakini mimi najua si bure kila kitu kilichoingia kitakuwa
kimetiwa baraka na mhariri wa tango hilo au la basi ni gumzo ambalo ingawa si
makini ni kichocheo cha fikira na watu wakilimeza bila taarifa mambo huenda
kuwa kama mlevi wa gongo.Na wapo watu wanaoamua kuwalewesha watu wengine.
Unapokuwa na watu wa aina hii ambao ndio mhimili wa taarifa za
dunia basi ujuwe walakini mkubwa upo labda kukosekana kwa namna bora ya
kuwasilisha hoja kwa kufuata mikondo inayoeleweka.
Unapokuwa na chuki binafsi masuala ya kizandiki lazima
yajichanue lakini unapokuwa humpendi fulani upuuzi wa kutunga uzushi lazima
utakuwepo na unapoona kuna kitundu tu kidogo unautangaza uwongo huo ambao
unakuwa mkubwa na unaokubalika kuliko shauri la majimaji alilolianzisha
kinjeketile kwa ajili ya kuwakomboa watu wake kutoka utumwani.
Rais Jakaya Kikwete wakati wa tuzo za uandishi mahiri,EJAAT,
hili nisiliseme aliasa waandishi wa habari waachane na uongo waandike ukweli,
waachane na chuki za kisasiasa wahabarishe wao ndio nguzo ya jamii,sasa mimi
nasema na tufanye utafiti wa kina kabla ya kukubali tuhuma zozote zile
tunazoambiwa:kwani inawezekana kabisa tupo ambao lazima tufe kwa staili yetu ya
maisha na pia lazima tufe kwa sababu tunadhani muda bado.
Nataka kusema tchao kwani mwenye akili na asiyekuwa na akili
kwa kawaida lao moja wanapishana digrii ya utekelezaji.
Subscribe to:
Posts (Atom)





















